GET /api/v0.1/hansard/entries/881136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 881136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/881136/?format=api",
"text_counter": 12,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwatate, ODM",
"speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": " Shukrani, Mhe. Spika kwa hii fursa. Nimesimama kuunga mkono malalamishi haya ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu. Ni leo tu asubuhi mkazi mmoja wa eneo Bunge langu amenitumia barua kwa njia ya nukishi akilalamika kwamba yeye ni mgonjwa na hali yake ni mbaya. Kwa wale ambao hawaelewi, nukishi ni fax . Ni kweli kwamba wengi wao ambao walistaafu mwaka wa 1997 walikuwa ni wazee na hela hii imechelewa. Ninaomba Kamati ambayo inashughulikia suala hili iharakishe. Mwaka jana mwezi wa tano, tulikutana na wale waliostaafu 1997. Wengi wao wamekomaa na ni wazee. Wanadai hela yao ambayo ni haki yao. Ingekuwa ni vyema hili suala liharakishwe vilivyo. Wengine walikuwa wanalalamika kwamba sehemu nyingine nchini watu wamepata hela zao ilhali wao hawajapata. Naunga mkono kwa dhati kabisa."
}