GET /api/v0.1/hansard/entries/881618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 881618,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/881618/?format=api",
"text_counter": 494,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitutu Chache South, FORD-K",
"speaker_title": "Hon. Richard Onyonka",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa, ikiwezekana, unipe fursa kuzungumza kidogo kuhusu mambo ambayo yametushinda katika nchi yetu. Nimesikia ndugu zangu hapa Bungeni wakizungumza kuwa wale wafanyikazi ambao wamefanya mgomo wafutwe kazi. Nimesikia ndugu zangu wakisema kuwa hata kama uongozi wa uwanja wetu wa ndege ni mbaya, wafanyikazi wasiulize maswali. Nimesikia ndugu zangu wakizungumza kiholela kwa hili Bunge ambalo wengine wetu tumekuwa kwa miaka mingi sana. Mambo yanayozungumziwa hapa leo ni mambo ambayo yanahusu nchi yetu ya Kenya. Lazima tuanze kuangalia masuala nyeti katika Bunge hili. Wananchi wameanza kutuona vibaya. Bunge hili limekuwa la kuongea ovyo ovyo. Masuala kuhusu migomo ya nchi hii ni masuala kuhusu uongozi wa nchi hii. Waalimu, wafanyikazi wa mahospitali na wafanyikazi wa viwanja vya ndege wanagoma.Ufisadi unafanya wananchi wagome. Lazima tuanze kujiuliza kazi iliyotuleta hapa Bungeni kama viongozi. Lazima tusikize vilio vya wafanyikazi wale. Lazima tuanze kujiuliza: Wale wafanyikazi waliogoma ni wazimu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}