GET /api/v0.1/hansard/entries/881990/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 881990,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/881990/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "(Trans Nzoia CWR, JP) : Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala huu ambao umeletwa na Mhe. Didmus, Mbunge wa Kimilili. Ningetaka kushirikiana na wenzangu ambao wanaunga mkono mjadala huu kuhusu nauli zinazolipishwa watu kwenye barabara zetu, hasa sekta ya uchukuzi katika nchi yetu ya Kenya. Vile Mhe. Dennitah Ghati ameongea hapa, kuhusu walemavu kutumia usafiri huu hapa nchini Kenya ni kweli kabisa. Baadhi ya hawa watu, hupata shida sana. Hii ni kwa sababu hawana nafasi ya kusimama ama kuongea na manamba wa matatu, na kusema wangependa nauli iteremshwe ama wanatoka pahali fulani wakielekea pahali pengine. Inakuwa ni huzuni kuona walemavu katika nchi hii wakiumia sana. Hasa ofisini zetu na wakisafiri kwenda mashinani kwenye kaunti zetu, huwa wanapata shida sana. Wenzangu hapa wameongea kuhusu washikadau katika sekta hii. Ndiposa mimi nakushukuru kwa kusema kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi katika Bunge hili akae hapa ili tuone pengo ambalo tunaweza kuziba katika kuhakikisha kwamba tumekuwa na usafiri bora nchini mwetu Kenya. Katika eneo la huko kwangu Trans Nzoia, utaona kwamba watu wenye matatu hawana nafasi hata ya kuegesha magari yao. Kaunti zetu hazijakuwa na mikakati mwafaka au jopokazi la kuhakikisha kwamba watu wa matatu wamepata nafasi zao licha ya kusema kwamba wanaweza kuwabeba wasafiri kutoka eneo moja kueleka maeneo mengine. Ndiposa mimi ninazisihi serikali zetu za kaunti na serikali kuu zihakikishe kwamba tumeweka mikakati mwafaka kuhakikisha kwamba wasafiri wamepata nafuu katika nchi yetu ya Kenya. Naweza kumnukuu Rais akisema kule Bomas of Kenya kwamba mambo ya ufisadi katika nchi yetu ya Kenya yamekita mizizi. Ndiposa unaona hata wahudumu na wenye matatu wana vyeo vikubwa serikalini na wengine ni askari. Uamuzi wa kusema nauli itakuwa namna gani ni wa mwenye matatu. Iwapo mwenye matatu ni askari, mwananchi wa kawaida atapata namna gani nafuu ya kuhakikisha kwamba anaweza kusimama mahali na aongee mambo ya nauli katika nchi yetu ya Kenya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}