GET /api/v0.1/hansard/entries/881991/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 881991,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/881991/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Sisi kama viongozi katika Bunge hili hatujakuja hapa ili kuzozana kama nilivyowaona wenzangu wakifanya. Baada ya mmoja kuongea, mwingine anamrushia matusi. Sisi sote tulikuja hapa sio kwa sababu tunafaa bali ni kwa mambo yake Mwenyezi Mungu kupitia kwa wapigakura kule mashinani kuhakikisha kwamba tuko hapa tukifanyia kazi wananchi waliotutuma katika Bunge hili. Mimi humpa kongole Rais mstaafu Moi ambaye alikuwa rais wetu kwa miaka 24 kwa sababu hawakusema alikuwa amehitimu kiwango fulani. Uongozi unamfaa mtu mwenye hekima zake za kuhakikisha kwamba anakuwa rais, kiongozi au katibu katika nchi yetu ya Kenya. Tukiwa katika Bunge hili tumetumwa na Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Didmus ni jukumu letu sisi kwa sababu tunapotoka mashinani, tunaona watu wakiumia sana. Ukija katika eneo la Trans Nzoia, kwa sababu ya uchumi na umaskini wa watu wa Trans Nzoia, utawaona wengi wakitumia pikipiki. Saa hii ninapoongea, wiki iliyopita mwalimu pamoja na wanafunzi wake waliokuwa wakisafiri kutumia pikipiki waligongwa na gari la serikali. Ndiposa ninasema lazima tuwe na mikakati mwafaka na hata jopokazi la kuhakikisha kwamba usalama na usafiri katika nchi yetu ya Kenya uko sambamba. Watoto wetu hutaka kusafiri kwenda shule au wanapofunga shule zao. Uliona hivi juzi kule Bungoma watoto wetu wakitumia matatu moja kutoka Bungoma kuelekea shuleni baada ya kutoka nyumbani na wakapata ajali katika barabara zetu na kupoteza maisha yao. Ndio tunasema huenda ikawa nauli iliteremka au ilipanda ndiposa watoto hao wakaamua kutumia gari moja. Ndio maana ninasema wacha tuwe na mikakati mwafaka ya kuhakikisha kwamba uchukuzi katika nchi yetu ya Kenya umeimarishwa. Naunga mkono wenzangu walioongea kuhusu barabara zetu. Hiyo ni kweli kwa sababu tunapoenda huko nje, tunapata kwamba barabara zao zimetengenezwa sambamba. Ziko sawa. Lakini ukija katika nchi yetu ya Kenya, wale ambao wamepewa nafasi ya kuhakikisha kwamba barabara zetu ni nzuri hawatumii nafasi hiyo vilivyo. Ndiposa unaona Wabunge wenzangu wakipigana katika Bunge hili wakisema hata Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ipewe hawa kwa sababu wanajua ni barabara zipi zina shida katika sehemu wanazotoka. Ndiposa nashukuru na kusihi magavana wanaochaguliwa katika serikali za kaunti wahakikishe kwamba wanaelewa masilahi ya watu wanaowashughulikia katika sehemu hizo. Namuunga mwenzangu aliyesema kwamba Mheshimiwa Didmus aje na Mswada katika Bunge hili. Akija na Mswada huo, itakuwa rahisi sana kwa sababu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi yuko hapa. Itakuwa rahisi sana kuangalia mapengo hayo ili tuhakikishe kwamba usafiri uko sambamba. Mheshimiwa mwenzangu ameongea kuhusu matapeli. Hapakosi matapeli katika kila sekta. Sio sekta hii peke yake ndiyo ina matapeli. Wanapatikana kila mahali katika nchi yetu ya Kenya. Lazima tuwe na mikakati ya kuzuia watu kama hawa katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu tunataka kuendelea mbele. Namshukuru Mheshimiwa Didmus. Nampongeza sana kwa kuleta mjadala huu katika Bunge hili ndiposa tuuchangie. Naunga mkono Hoja hii."
}