GET /api/v0.1/hansard/entries/882090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 882090,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/882090/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Spika. Ninataka kukubaliana na Naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kwa sababu ni ukweli ya kwamba tulikuwa na mkutano na tulijadilia maswala ambayo yametajwa hapa. Pia, amesema yakwamba tutazingatia mambo ambayo yametajwa hapa. Seneta wenzangu wanasema ya kwamba ni kama alikunywa chai na hakukua na mkutano ambao ulipaswa kufanyika. Sio ukweli alivyosema Sen. Cherargei ya kwamba tulijua ya kwamba haya maneno yangefanyika. Tulijadiliana hayo mambo kwa sababu hayo ndiyo mambo ambayo tunayafuata na tunayatekeleza kama Kamati. Kwa hivyo, hatuwezi kusema ya kwamba Naibu wa Mwenyekiti alifanya jambo la makosa. Tulikuwa tukitekeleza kazi ambazo tunapaswa kutekeleza na tutaendelea kutekeleza kwa mjibu wa sheria zilizoko katika Katiba yetu."
}