GET /api/v0.1/hansard/entries/882225/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 882225,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/882225/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kadiri ya vile tunavyoelewa ni kwamba ndege za Boeing zimeweza kupigwa marufuku kutua katika viwanja vya maeneo ya Uropa. Hii ni kumaanisha ya kwamba kule wameona kuna sintofahamu kidogo katika ndege hizo. Bw. Spika, kwa hivyo ingekuwa muhimu sisi kama Wakenya ambao tulipata madhara makubwa--- Nafikiria katika ndege hii waliopoteza watu wengi zaidi ulimwenguni ilikuwa ni Wakenya. Hii ni kwasababu walikuwa wanatarajia kufika nyumbani salama salimini kuungana na wapendwa wao. Kwa sababu hiyo, ingekuwa muhimu sana kama nchi yetu pia ingechukua hatua hiyo kama ilivyochukuliwa na nchi za Ulaya ya kwamba ndege yenye muundo huo wa Boeing 737 Max 8 ipigwe marufuku kupita katika anga ya nchi yetu. Inafaa wasubiri mpaka tupate taaarifa kutoka kwa wale Boeing wenyewe kwamba wamefanya uchunguzi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}