GET /api/v0.1/hansard/entries/882295/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 882295,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/882295/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ninataka kumshukuru Sen. Khaniri, kwa Statement ambayo ameleta. Ningependa kusema kwamba mimi nikiangalia kwa marefu na mapana mambo haya yameangaziwa vizuri; yote ni ukweli mtupu. Kenya kumekuwa na vikundi vingi na kwanza kabisa ninataka kutuma risala zangu za rambirambi kwa wale waliovamiwa pale Kililingili. Ninasema, pole sana kwao. Lakini ukiangalia Kenya kuna vikundi vingi kama vile Mungiki, Chinkororo na vinginevyo. Vikundi hivi vimekuwa vikiongezeka sana kwa sababu ya ukosefu wa kazi kwa vijana wetu. Ninataka kukemea hivi vikundi kwa sababau ukitembea, kwa mfano, kule Laikipia, utapata kuna vikundi vingi, hasa kikundi cha Mungiki. Kuna jambo ambalo linanitia hofu, kwa sababu, unapata kwamba, wale ambao wanasemekana wanaongoza hivi vikundi, wakati wa uchaguzi tunaitishwa stakabadhi ili kuonyesha kwamba tumehitimu kusimama. Unapata kwamba wagombeaji viti wengine ni washukiwa au ni viongozi wa hivi vikundi. Kwa hivyo, ninaona Serikali haijajitolea kabisa kupambana na hivi vikundi. Askari wamezembea katika kazi zao kwa sababu watu wanaibiwa, wananajisiwa, watoto wanalaitiwa ilhali ni karibu na vituo vya maafisa wa usalama. Maafisa wa usalama wenyewe wanaonekena kuzembea katika kazi yao. Ikiripotiwa unasikia wakisema ya kwamba, unapaswa uwashike wale watu; uwalete. Unashindwa kazi yao ni ipi. Kazi yao ni kuketi pale kungoja, lakini kukiskika mahali watu wamekunywa pombe, wanataka kuenda pale kuitisha mlungula, lakini wanahitajika kupigana na hawa wakora, askari wenyewe hawapatikani. Kwa hivyo ningeomba, Serakali yetu ya Jubilee - amabayo nimeskia ikikashifiwa - tufanye kazi tukiwa kitu kimoja kwa sababu kuna yale mapatano. Kama kuna ufisadi, sisi sote tuwe pamoja. Kwa hivyo, ni vizuri tuungane tufanye kazi tukiwa pamoja na tuwache kukemea wenzetu kwa sababu utengano ni udhaifu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}