GET /api/v0.1/hansard/entries/882722/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 882722,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/882722/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kuchukua fursa hii pia kuunga mkono mwenzangu kuhusu mjadala huu kuhusu mambo ya ugonjwa wa kisukari katika nchi yetu ya Kenya. Ni ukweli vile wachunguzi wamesema kuhusu asilimia ya watu ambao wanaugua ugonjwa wa kisukari. Ni ukweli mtupu. Ningeomba kama kiongozi kwamba tuwe na mahali ambapo watu wanaweza kufanyiwa uchunguzi ili wajue hali yao iko namna gani. Vile mwenzangu, Mhe. Tom, amesema, ni kweli ukienda kule mashinani watu hawajui maana ya kupima miili yao. Hivi juzi nilikutana na mmoja wao aliyekuwa akiugua ugonjwa wa kisukari na nikamuuliza kama ameenda kupata matibabu. Alinijibu akasema kwamba yeye hunywa pombe ya chang’aa na ana imani kwamba ugonjwa huo wa kisukari utaisha. Ni muhimu sana tuwahamasishe watu wanaougua ugonjwa wa kisukari katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu kuna wengi wasiojimudu kimaisha ambao wanakaa katika maisha ya upweke na hawana fedha za kwenda kujipima kama ni wagonjwa au si wagonjwa."
}