GET /api/v0.1/hansard/entries/882724/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 882724,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/882724/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "hawajaenda katika hospitali zetu kujipima. Ninaungana na wenzangu. Serikali yetu kuu ichukue nafasi yake kuhakikisha kwamba matibabu ambayo tunayasema kuhusu watu wanaogua kisukari yametiliwa maanani. Wenzangu pia wamesema watu wawe wanaspoti, yaani wafanyie miili yao mazoezi. Ninashukuru kwa sababu wanaspoti katika Bunge hili wakati tulienda mazoezi na viongozi wenzetu, tuliona kwamba nchi zingine zinatenga nafasi za watu wao kwenda kufanya mazoezi. Hiyo inatupatia sisi nafasi ya kuhamasisha watu wajue kwamba miili yao inatakikana ifanye mazoezi ili wasikumbwe na mambo kama haya. Hata katika Bunge hili, kuna wale ambao wameathirika miongoni mwetu sisi kama viongozi. Huenda ikawa wengine hawajajua wachukue nafasi gani ama wafanye namna gani ndiposa angalau wapate nafuu katika miili yao."
}