GET /api/v0.1/hansard/entries/882725/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 882725,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/882725/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Ninamshukuru Mhe. Ruweida kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili nasi pia tutoe maoni yetu. Ninajua kwamba hata tukienda mashinani, sisi pia tutapata nafasi. Ninashukuru kuna madhehebu katika nchi yetu ya Kenya, kama vile kanisa la Seventh Day Adventist (SDA), ambayo yana vipimo vya kupima magonjwa katika kanisa hilo. Ninawasihi wachungaji katika nchi yetu ya Kenya watusaidie katika sehemu zao kuhakikisha kwamba vipimo hivi vimeenda mahali hapo. Jambo hilo litatusaidia sana. Nikirudi kwa serikali za kaunti, katika kaunti yangu, watu wanateseka mno. Ukienda sehemu za Kwanza ambako Mhe. Ferdinand anatoka, unaona kwamba tumepoteza watu wengi mno wanaougua ugonjwa wa kisukari na huenda ikawa viongozi mashinani wanatungojea sisi katika Bunge kuu au Serikali kuu kuhakikisha kwamba tunafikisha dawa kule chini. Sio ugonjwa wa kisukari pekee. Wengi pia wana ugonjwa wa saratani katika miili yao. Itakuwa vyema iwapo tutakuwa na uhamasisho wa watu jinsi ya kujichunga na kujipima. Itakuwa vizuri sana. Inakuja kwa mambo ya maisha kwa sababu wengi wanataka kula chakula cha mafuta lakini hapo awali mababu na mama zetu enzi zile walikuwa wanatafuta chakula cha kujenga mwili wala sio chakula cha kutufanya wanene au wembamba. Wengine hufikiria kwamba ukiwa na ugonjwa wa kisukari utakuwa mnono. La! Kuna wale ambao wamekonda na wana ugonjwa huu wa kisukari. Ndio tunasema ni muhimu tuwe na hivyo vipimo ili watu wajue vile wanaugua. Hii itatuwezesha kuhakikisha kwamba tunaishi maisha mazuri katika nchi yetu ya Kenya. Pia, kama viongozi, tutapata nafasi nzuri na kuhamazisha watu wetu mashinani kuhakikisha kwamba wanapata matibabu."
}