GET /api/v0.1/hansard/entries/883163/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 883163,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/883163/?format=api",
    "text_counter": 403,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Nasimama hapa kuunga mkono Ripoti hii ya Kamati. Ukuta huu utasaidia sana. Tuulizeni sisi watu wa Lamu kwa sababu tuliumwa. Sasa tunajua umuhimu wa ukuta huu lakini tunazungumzia ukuta sio fence . Jana nilikuwa Ishakani na Kiunga. Niliona kontrakta anatengeza miti yani poles . Sikuona kama wanatengeneza ukuta. Ni vile wenzangu walivyozungumza kwamba si ukuta ni fence . Pia, naomba ikiwa watajenga ukuta, na Mwenyekiti wa Kamati alijitetea kwamba kwingine kutakuwa ni ukuta na kwingine ni waya, kuhakikishwe kwamba jamii ya Wabajun kwenye mpaka ishughulikiwe. Kuna Wabajun wa Somalia na wa Kenya. Waweke zile nafasi ambazo wataweza kupita ili wahamiaji ama wasafiri wasikatazwe ila waweze kuja. Hizi ni jamii ambazo ziligawanywa. Nataka kuzungumzia zaidi hii Southern Sector - Libat-Kiunga ambayo ni kilomita 105. Ni muhimu iwekwe ukuta sawa sawa. Ukuta huo utasaidia sana kwa sababu kule Boni kuna mambo huwa yanatokea. Kulingana na Kamati, ukuta huo ulikuwa uwe tayari. Ni matarajio yetu kwamba utakuwa tayari mwaka huu. Unafaa uwe umemalizika mwaka huu. Unafaa uwe umemalizika kitambo kwa sababu zile shida tunazozipata sisi watu wa Lamu zinatufanya sisi viongozi wakati mwingine hatuwezi kufanya kazi yetu. Kamati ya Regional Integration ya Bunge ilienda ikakatazwa kufika Kiunga. Saa hii, shule tano za Basuba Ward zimefungwa. Hakuna shule. Hiyo jamii mpaka sasa hawana hata mtu mmoja ambaye amemaliza chuo kikuu. Ikiwa shule tano zitafungwa basi sisi tutakataa ukuta? Tutofautishe wale wahalifu wa kutumia pesa hiyo vibaya na ukuta. Hiyo ni kesi tofauti. Wale wahalifu wasisababishe mambo mazuri kutofanyika. Kama kuna uhalifu ni jukumu la Bunge hili lihakikishe hao wahalifu wameshikwa lakini ukuta uwekwe. Nimependa mapendekezo mengine ya Kamati hii. Kamati imesema ule uwanja wa ndege uondolewe Kiunga uwekwe mwingine. Ni matarajio yetu kwamba wataujenga uwanja mzuri lakini Kamati imesema kwamba itahusisha viongozi. Mimi ni kiongozi wa Lamu lakini bado sijahusishwa. Sijui ni viongozi gani wanahusishwa. Pendekezo lingine ni kwamba barabara ya Hindi-Bodhei-Kiunga iwekwe lami. Ni muhimu ikiwekwa lami kwa sababu asilimia 10 ya uhalifu utapungua. Kabla lami iwekwe angalau wangefyeka pande zote mbili za barabara ili wale wahalifu wakitokezea waonekane. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}