GET /api/v0.1/hansard/entries/883164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 883164,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/883164/?format=api",
    "text_counter": 404,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Tumetoa maoni hayo mara nyingi. Lakini sijui kwa nini ukiwaambia wafyeke hawafanyi hivyo bali wanaenda kugusagusa kidogo na hawamalizi kazi hiyo. Nashangaa anasema kwamba ameenda Mandera. Kamati itueleze zaidi kwa nini hawakuanza na Lamu na wanajua sisi ndio tunapata matatizo zaidi. Mbona wasianze Lamu? Naomba Kamati hii ije Lamu ione. Iende Kiunga na Ishakani. Kamati imependekeza kwamba kontrakta watajwe kwa sababu nimeenda Ishakani na hawana maji ilhali kontrakta ako pale anajenga mambo yake. Si ubinadamu. Huyo kontrakta angesaidia ile jamii angalau na gari moja ya maji kwa wiki. Kontrakta anajenga pale na watu wanaumia na hawezi hata rejesha maji kwa jamii. Kama ni mtu wa pale pale, tumjue na kama ni mwingine, tumjue mkandarasi ni nani ili awasaidie wale wananchi. Kama nilivyotangulia, ni changamoto kwa sisi viongozi pia. Kuna sehemu Lamu hatuwezi fika kwa sababu ya utovu wa usalama. Mimi nashangaa watu wakisema ukuta usiwekwe. Ukuta uwekwe lakini wahalifu washikwe."
}