GET /api/v0.1/hansard/entries/883654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 883654,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/883654/?format=api",
    "text_counter": 483,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, Mswada huu pia unatoa mwongozo kwamba kanuni zitakazopitishwa zitabatilishwa baada ya miaka kumi kutoka ile tarehe ambayo zimepitishwa. Tunaona kwamba kaunti nyingi zina kanuni za kutoka wakati wa Mwingereza. Kanuni zile zimetumika kutoka wakati wa Serikali ya ukoloni. Ukiangalia katika kaunti nyingi, kanuni zote zinazohusiana na ujenzi wa majumba zilitengezwa wakati wa ukoloni. Kwa hivyo, sheria hii inatoa mwongozo kwamba zile kanuni zinakufa baada ya kila miaka kumi. Pia, sheria hii inapendekeza kwamba zikifa, lazima aidha ziongezewe muda, na muda utakaoongezwa hautazidi miezi kumi na miwili; ama kanuni zingine mpya zipitishwe kuhakikisha kwamba zinaambatana na sheria. Vile vile, kama zitaongezwa kwa muhula wa miezi kumi na miwili, itakuwa zinaweza kuongezwa mara moja peke yake. Kifungu cha 18(4), kinasema kwamba muda unaweza kuongezwa. Yaani muda wa miaka kumi unapokwisha, inaweza kuongezwa muda wa mwaka mmoja peke yake, wala sio zaidi ya hapo. Kwa hivyo, hiyo ni sheria nzuri ambayo lazima tuiunge mkono."
}