GET /api/v0.1/hansard/entries/885106/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 885106,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885106/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, kwanza nataka kumshukuru ndugu yangu, Seneta Khaniri, kwa Statement aliyoleta. Katika maeneo ninayotoka ya Kilifi na pwani kwa ujumla, kuna watu wa tabaka mbalimbali. Kwa hivyo, cheti cha kuzaliwa ni cha umuhimu sana. Jambo la kwanza ambalo ningependa kusema ni kwamba Serikali inafaa kuondoa ada ya vyeti vya kuzaliwa. Kupata cheti cha kuzaliwa inafaa kuwa ni haki ya kila Mkenya. Wakati mtu anapozaliwa, hakuna haja ya kuandika barua ya kuomba cheti cha kuzaliwa."
}