GET /api/v0.1/hansard/entries/885109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 885109,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885109/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Utoaji wa vyeti vya kuzaliwa umekuwa chombo cha kutafuta pesa miongoni mwa wafanyakazi wa afisi zinazotoa huduma hiyo. Mara nyingi, utapata mtu anaitishwa “kitu kidogo” ili fomu yake ipitishwe. Hii ni tabia inayoendelezwa na maafisa wanaofanya kazi katika ofisi za kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa sababu ufisadi umekithiri na hiyo imekuwa biashara kubwa. Hali hiyo inaathiri jamaa zetu ambao, kama nilivyosema hapo awali, ni ndugu zetu wa dini ya Kiislamu. Wengi wa wale ninaowakilisha ni Waislamu. Hii ni kumaanisha kwamba si rahisi mtoto wa Kiislamu kupata cheti cha kuzaliwa ikilinganishwa na mtoto wa Kikristo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}