GET /api/v0.1/hansard/entries/885110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 885110,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885110/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ni aibu kumtaka mtoto ambaye wazazi wake ni Wakenya alete cheti cha kuzaliwa cha babu yake. Kwa nini mtu atake cheti cha kuzaliwa cha nyanya yangu? Ni sawa ukitaka nikuletee cheti cha kuzaliwa cha mamangu na babangu, lakini sio vizuri kuanza kuulizwa aliyemzaa babu yako ni nani na anatoka wapi. Sisi sote sio wenyeji wa nchi ya Kenya. Historia inatuonyesha kwamba watu wengi walikuja wakakutana hapa, na sote sasa ni watu tunaoishi katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, ni makosa kwa serikali yetu kufanya biashara kwa kutumia cheti cha kuzaliwa. Ukienda kutafuta cheti, utaambiwa ulipe Kshs100 au Kshs200 na usipokuwa na cheti cha kuzaliwa cha mama yako au cha babu yako, utaambiwa kadri ya pesa unazohitaji kulipa. Mimi nilienda katika hizo ofisi na niliambiwa kwamba; ‘kama unataka huyu mtu wako apate cheti, basi tupatie Kshs30,000,’ Niliwaambia, ‘Huyu ni Mkenya na tumeishi naye pamoja. Najua alipozaliwa na kila kitu chake kinajulikana. Kwa nini alipe Kshs30,000, ilhali mtoto mwingine ambaye ni mkristo asilipe?” Mwishowe, alipata cheti hicho, lakini ilikuwa shida sana kukipata. Inafaa watu walioko katika maofisi ya kutengeneza vyeti vya kuzaliwa waache mambo ya ufisadi. Sisi sote hatuna wazazi wanaoweza kulipa pesa ndiposa tuzaliwe hospitalini. Kwa mfano, mimi sikuzaliwa hospitalini; nilizaliwa kule vijijini ninakotoka."
}