GET /api/v0.1/hansard/entries/885112/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 885112,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885112/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Ndugu yangu anasema ya kwamba kunaitwa kichochoroni, lakini sio kichochoroni; ni kule mashambani. Itakuwa matusi kama mimi nitapewa cheti, na mtu mwingine ambaye amezaliwa huko hawezi kupewa kwa sababu ya dini yake. Itakuwa makosa kwa sababu Katiba yetu inasema ya kwamba usimbague mtu kwa sababu ya dini, rangi au mahali anapozaliwa. Ikiwa mtu huyo anatetewa na Katiba, sioni sababu ya wafanyikazi katika ofisi zile kuleta shida. Tulipokuwa na shambulizi katika DusitD2, Wakenya waliwatetea wale ambao walikuwa pale. Hatukubaguana kwa msingi wa ukristo ama uislamu; na hatukusema ya kwamba, “Huyu hana dini ama ni Muhindi.” Wakenya walijitokeza na kuhakikisha ya kwamba kila mtu yuko sawa, ama amepelekwa hospitali ya karibu. Watu walitoa magari yao bila kuuliza, “Wewe ni wa dini gani; ama wewe ulizaliwa wapi?” Ilisemwa ya kwamba kila mkenya ambaye alikuwa ameumia apelekwe hospitali. Kwa hivyo, tusifanye biashara na vyeti vya kuzaliwa."
}