GET /api/v0.1/hansard/entries/885172/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 885172,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885172/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13156,
"legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
"slug": "mutula-kilonzo-jnr"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii kuwakaribisha wanafunzi wa shule ya Upili ya Thomeandu. Wacha nikurekebishe kidogo, kwa sababu wewe ni Mbantu kama mimi, na hungeweza kulitamka jina “Thomeandu” vizuri. Jambo la pili, namshukuru Sen. Sakaja na Sen. Madzayo kwa kusema kuwa mavazi yangu yanapendeza. Tatu ni kuwakaribisha wanafunzi wa shule ya upili na mwalimu wao mkuu, ambao tumefanya kazi nao pamoja kwa ukaribu. Kwa sababu majirani wao ni wanafunzi wa Precious Blood, Kilungu, wamekuwa wakishindana; na jambo hili limefanya wanafunzi hawa wafanye vizuri katika masomo yao. Wamefanya vizuri kwa kuja katika Bunge la Seneti, wakiwa wametoka Bunge la Kitaifa, ili wajijulishe mambo tunayoyafanya. Bw. Naibu Spika, nawasihi ndugu na dada zangu Maseneta wawakaribishe wanafunzi kutoka katika shule za kaunti zao. Hii ni kwa sababu wanapata nafasi ya kuwaona viongozi wao, kujua historia ya Kenya yetu, Bunge letu na Bunge la Kitaifa. Hili ni jambo ambalo sisi wenyewe tunalichukulia kwa urahisi, lakini kwa watoto hawa, ni jambo la maana sana. Rais mstaafu, Bill Clinton, alipata ari ya kuwa Rais wa Marekani siku ambayo yeye na wanafunzi wengine walipata nafasi ya kutembelea Bunge lao. Kuna uwezekano kuwa pengine tutapata rais na viongozi wengine kutoka katika wanafunzi wanaotembelea Bunge letu na lile la Kitaifa. Jambo la pili ni kuhusu matamshi ya Sen. Sakaja, Seneta wa Kaunti ya Nairobi, kuhusu nidhamu; hili ni jambo muhimu sana. Wanafunzi wa shule ya Upili ya Thomeandu, mavazi yako ndiyo yanayoonyesha nidhamu yako. Karibuni sana."
}