GET /api/v0.1/hansard/entries/885461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 885461,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885461/?format=api",
"text_counter": 467,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "ikiwa ni chakula - na wao wanaishi katika jangwa huko Israeli - hakuna anayepoteza maisha. Ilhali sisi udongo wetu ni udongo ambao unaweza kuleta chakula na tukapata chakula kingi na hatuoni ni kwa sababu gani, ndani ya nchi yetu ya Kenya, kwamba Mkenya anaweza kupoteza maisha yake kule Turkana. Bi Naibu Spika wa Muda, hatuulizi ya kwamba sisi kama wakenya, hatubahatishi, ama hatuwezi kusema ya kwamba tuna bahati ya kuishi Kenya ama tunaomba tuishi Kenya, ili tufe. Hao hao mabwanyenye ambao wanafanya mambo ya ufisadi, ndio hao hao, hivi sasa wenye mabloki ya mafuta uko; sijui yanaitwa Ngamia block, wamerurumana huko wanachukua Ngamia ili wachukue mafuta ya waturkana. Turkana ina maji, mafuta na wakaazi wake, lakini leo utapata ya kwamba waturkana ni kama ambao sio Wakenya. Wanakufa na mafuta yao na maji yao. Ni kwa nini Serikali haiwezi kuchukua hatua mara moja kuona ya kwamba yale maji yaliyo chini ya ardhi ya Turkana yameweza kuchimbuliwa yakapatikana na watu wa Turkana wakaishi wakiwa na maji mengi hata zaidi kusaidia pande zingine za Kenya. Ama vile vile pia, kuweza kupata mafuta ya kuweza kujikimu kimaisha na kuendeleza maisha yao. Bi Naibu Spika wa |Muda, tunataka Rais, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta atangaze hii njaa kama hatari kubwa ndani ya taifa letu la Kenya. Ya kwamba, watu waache kufanya kazi zote sasa. Ninakubaliana na ndugu yangu, mkubwa wangu mwanasheria maarufu sana katika Kenya, Sen. Wetangula, ya kwamba, sasa Serikali na hata serikali zetu za mashinani katika ugatuzi, ziwache kufanya kazi zozote hivi sasa na kuangalia hili janga la njaa. Kule Kilifi tuna shida kama hiyo pia. Na wao pia waache kufanya kazi zingine sasa ili waangalie baa la njaa ambalo liko ndani ya maeneo Bunge ya Ganze na Magarini na maeneo yote ambayo yamepatikana na baa la njaa, ikiwemo mojawapo katika Kenya, kule Turkana na hata Baringo. Ni aibu kuona mahali ambapo paliongozwa na Mheshimiwa Rais mstaafu wa Kenya, Mheshimiwa Daniel Arap Moi, leo watu wake wanakufa njaa na Serikali ya Kenya ikiwa inatawaliwa hapa haiwezi kufanya chochote kuona ya kwamba yule Mkalenjin anayeishi kule ndani ya Baringo hawezi kuboreshwa katika maisha yake kwa kupata chakula. Aibu kama hii inaonyesha kwamba hii Kenya tuna kasoro ambayo inaletwa na wale ambao ni wezi ndani ya Serikali."
}