GET /api/v0.1/hansard/entries/885503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 885503,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885503/?format=api",
"text_counter": 509,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Sasa hivi ukimwuliza gavana yeyote kutoka maeneo yaliyoathirika, atakwambia anatafutia watu wake chakula. Hili ni jambo la kuvunja moyo kwa sababu tulidhania kuwa ugatuzi utafanikisha watu kuwa na chakula. Sasa hivi, kila mtu ananyooshea Serikali ya kitaifa kidole. Inafaa magavana na hata maseneta waelezee watu wanachofanya. Najua kuwa hata Laikipia kuna shida kwa sababu nimekuwa nikiambiwa. Mimi mwenyewe nina jukumu la kufuatilia jinsi Gavana anatumia hela zinazofaa kutumiwa wakati wa dharura. Hata hivyo, Serikali ya kitaifa ina jukumu kwa sababu mwaka jana kuna taasisi za Serikali zilizotutahadharisha kutokana na hali ya hatari. Tuliambiwa kuwa kutakuwa na athari za ukame lakini Serikali haikufanya chochote."
}