GET /api/v0.1/hansard/entries/885523/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 885523,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/885523/?format=api",
"text_counter": 529,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya Seneta wa Kaunti ya Bungoma, Sen. Wetangula. Bi. Spika wa Muda ningependa kutilia mkazo kwa yale yote yaliyozungumziwa hapa. Hakuna linguine ambalo linaloweza kuongezewa bora kuliko kusema kwamba, ni lazima sasa hatua za kinidhamu zichukuliwe. Haya yaliyotendeka yote, watu kufa kwa njaa na kuishi katika hali ya uchochole katika sehemu nyingi kama Baringo, Kilifi, Tana River, Kwale na Kinango; kuna uchochole kama huu unaoendelea katika eneo la Turkana. Kwa hivyo sasa inapaswa hatua za kinidhamu zichukuliwe, watu washtakiwe na wachukuliwe hatua wafungwe, ili iwe ni funzo kwa watu wengine watakaokuja baadaye. Bi. Spika wa Muda hakuna haja kuwa na Serikali ambayo in Katiba inayosema kwamba watu wana haki ya kupata chakula ama kuishi bila njaa, wakati watu wanakufa na njaa katika karne ya ishirini na moja. Miaka hamsini na tano ya Uhuru imekuwa kama ni mchezo sasa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}