GET /api/v0.1/hansard/entries/886033/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 886033,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/886033/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Statement ya Sen. Malalah kuhusu vita dhidi ya ufisadi. Ni lazima tupambane na ufisadi kwa sababu ufisadi umekuwa donda sugu katika nchi yetu. Kila mwaka tumekuwa tukilalamika kuhusu ufisadi lakini hatujaona matokeo yoyote ya vita dhidi ya ufisadi. Tumekuwa na taasisi kadhaa za kupambana na ufisadi kama vile Kenya Anti-Corruption Commission (KACC) na EACC lakini hatujaona matokeo ya kazi zake. Mwaka huu, kidogo kazi imeanza kufanywa. Kama ilivyo kawaida, lazima wanasiasa walete siasa mahali ambapo hakuna siasa. Yeyote anayetuhumiwa kwa ufisadi ana haki ya kwenda mahakamani na mahakama ina fursa ya kuangalia kesi na kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Kwa hivyo, hakuna sababu ya watu kupinga vita dhidi ya ufisadi. Ikiwa mtu anatuhumiwa kwa madai ya ufisadi, ni vyema kujiuzulu mamlakani ili uchunguzi ufanywe. Endapo atapatikana bila makosa, ana haki ya kuendelea kufanya kazi yake. Ukitoa madai kuwa mimi ni mfisadi, una haki ya kutoa ushahidi utakaochunguzwa na mahakami ili ukweli upatikane. Tusitupie mawe ofisi za DCI, EACC na DPP kwa sabubu ya tuhuma za ufisadi dhidi ya jamaa zetu. Uchunguzi unafaa kufanywa na wale watakaopatikana na hatia wapelekwe mahakamani. Bi Spika wa Muda, juma lililopita, tulikuwa na mkutano na maafisa wa DCI, EACC, pamoja na Mkuu wa Sheria. Wote walisema kwamba vita dhidi ya ufisadi havina kabila, jamii, wala sura ya mtu yeyote. Kwa hivyo haiwezi ikaonyesha ya kwamba hawa ndio wanaotumiwa kwa ufisadi. Kwa hivyo, ni lazima tuunge mkono vita dhidi ya ufisadi. Zile pesa zinazoliwa kwa ufisadi zingeweza kutumika kufidia watu ambao wamepata shida ya ukame. Hilo halitendeki kwa sababu tunajaza matumbo yetu nakusahau maskini ambao wametuleta mamlakani. Tunaendelea na ufisadi na ndio maana nchi yetu iko katika hali atiati."
}