GET /api/v0.1/hansard/entries/886058/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 886058,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/886058/?format=api",
    "text_counter": 184,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, Bandari ya Mombasa ni kiungo muhimu katika uchumi wa kaunti za Pwani hususan Mombasa. Asilimia kubwa ya watu wa Pwani wanategemea Bandari ya Mombasa kwa njia moja au nyingine. Hivyo basi, mama mboga anatarajia mfanyikazi wa bandari kununua mboga zake jioni. Dereva wa lori anatarajia kubeba makasha kutoka Bandari ya Mombasa na wauzamaji barabarani pia wanapata biashara kutokana na bandari hiyo. Bi. Spika wa Muda, mchakato huu wote unaleta mapato kwa kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi, Taita Taveta, Kajiado, Makueni na Machakos. Iwapo biashara bandarini itapungua, mapato ya kaunti hizi yataathirika kwa sababu kaunti hizi zinategemea pakubwa mapato ya biashara pamoja na pesa zinazotoka kwa Serikali Kuu. Bi. Spika wa Muda, japokua Bandari ya Mombasa imepanuka pakubwa na kujenga kituo cha kisasa cha kupokea makasha yani container terminal na pia ina reli mpya ya StandardGauge Railway (SGR ), kusafirisha makasha kutoka bandarini hadi sehemu zingine nchini, wakaazi wa Mombasa wameathirika pakubwa na maendeleo haya kwa sababu hawapati faida yoyote kwa bandari hiyo na kwa shirika ambalo haliwajibikii Mombasa kwa njia yeyote. Bi. Spika wa Muda, swala la ajira kwanza limekuwa donda sugu. Ijapokuwa makao makuu ya Shirika la Bandari ni Mombasa, wakaazi wa Mombasa hawapati ajira kutoka kwa shirika hilo. Hakuna uwazi katika uwajiri katika Shirika la Bandari la Mombasa. Vile vile, kituo kipya cha makasha kinafanya kazi hivi sasa lakini asilimia 70 ya wafanyikazi walioajiri sio wakaazi wa Mombasa. Vilevile, wakaazi wa Mombasa wamepokonywa biashara. Makasha yakiteremshwa katika meli, yanapakiwa moja kwa moja kwenye reli au mabohari ya SGR na kusafirishwa moja kwa moja hadi Nairobi. Hii imesababisha kampuni hizo kufunga biashara. Madereva wengi na wasaidizi wao wamekosa ajira na hii imesababisha mapato ya kaunti kupungua kwa asimilia kubwa, kwa sababau haya mashrika hayataweza kulipa ushuru kwa Kaunti ya Mombasa. Bi. Spika wa Muda, vile vile, zile kaunti jirani ambazo zinategemea biashara pia; biashara hiyo imepungua. Serikali Kuu haijatoa mwongozo ni vipi wafanyi biashara watalipwa ridhaa kwa hasara wanazopata wala kupewa miradi mbadala kuendeleza biashara zao. Bi. Spika wa Muda, tumeona katika sehemu nyingine nchini,wakaazi wakifadhiliwa pakubwa na Serikali. Kwa mfano, Serikali ya Uingereza ilipopiga marafuku kuingizwa kwa Miraa nchini humo, Serikali ilitoa pesa nyingi kuwafidia wakulima wa miraa katika sehemu zile zinazokuza miraa. Vile vile, viwanda vya sukari, ambavyo vingi viko katika hali mahututi; vimefadhiliwa pakubwa na mabilioni ya pesa na Serikali ili kuwalipa wakulima wa miwa. Mipango kama hii haijakusudiwa katika Kaunti ya Mombasa wala kuwasaidia wakaazi kwa jambo hili. Jambo la kuhuzunisha kabisa ni kwamba Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Macharia, alijipiga kifua akisema kwamba amefaulu kuyaondoa magari 3,000 ya mizigo barabarani, na hivyo kuwafuta kazi zaidi ya watu 6,000 waonaotegemea kazi hizo. Bi. Spika wa Muda, hatukatai kwamba reli ya SGR imesaidia pakubwa biashara ya kuleta makasha Nairobi. Kitu ambacho tunasema ni kwamba lazima SGR iruhusiwe kufanya biashara sawa na wafanyi biashara wengine, kwa mfano; biashara ya kusafirisha mizigo, isitolewe kwa"
}