GET /api/v0.1/hansard/entries/886062/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 886062,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/886062/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "ruhusa ya kupeleka mizigo hiyo kwa zile CFS ambazo zilikuwa zimefunguliwa kupunguza msongamano katika Bandari ya Mombasa. Bi. Spika wa Muda, tuna changamoto nyingi Mombasa. Kuna changamoto za kiusalama, madawa ya kulevya, itikadi kali na ugaidi, uhalifu wa aina mbalimbali; na isipokuwa hatuna ufisadi wa hali ya juu kama vile wizi wa pesa za mabwawa, matatatizo mengi ni ya kijamii. Jiji la Mombasa linaendelea kufa polepole na iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa, mji utakuwa gofu. Biashara ya utalii ilikufa zamani . Sasa utalii uliopo ni wakenya kutoka sehemu nyingine nchini kutembelea Mombasa. Hii Bandari ndio tegemeo kubwa. Mradi wa Dongo Kundu Special Economic Zone, bado umekuwa ndoto kwa watu wa Mombasa. Iwapo mradi huu utafanywa kwa haraka, itasaidia pakubwa kuongeza mapato ya Kaunti ya Mombasa. Kwa hivyo napendekeza suala hili lipewe kipaumbele na uzito."
}