GET /api/v0.1/hansard/entries/886076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 886076,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/886076/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13119,
"legal_name": "Agnes Zani",
"slug": "agnes-zani"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Kwanza nawasalimu na kuwakaribisha wageni wetu wa Chuo Kikuu cha Tangaza. Hili ni Bunge la Seneti ambapo tunayazungumzia mambo katika kaunti zetu. Leo tunalizungumzia jambo muhimu ambalo limeletwa na Sen. Faki. Nataka kumshukuru Sen. Faki kwa kuleta taarifa hii ambayo inahusu hali ya uchumi za kaunti ambazo ni jirani na Kwale. Kaunti hizi ni Mombasa, Kwale, Kilifi na Taita Taveta. Ni kweli na ni kwa muda mrefu, tunatoa kilio kuhusu Bandari yetu, vile ambavyo mambo yamefanywa, kwamba sasa bidhaa zikifika zitaekelewa kwa magari, ziletwe upande wa Naivasha. Katika hali hii, mambo kama ajira yanahusika, watu wa Mombasa na Kwale, sasa hawapati kazi kwani Bandari ndio ilikuwa mahali bora na mahali pa kwanza ambapo watu walikuwa wakitafuta kazi. Mambo yameenda kombo upande wa biashara kwa sababu Bandari ilipokuwa ikifanya kazi, watu wa Kwale na Mombasa walipata manufaa. Kulikuwa na biashara nyingi ambazo zilikuwa zinaendelea. Kwa upande wa utalii, pia hapo tumepata shida. Kwa jumla, ingawa Bandari lile ni la kujivunia kama watu wa Mombasa na watu wa kaunti jirani kutoka Kilifi, sasa limekuwa kama donda sugu. Limekuwa ni kwamba ni watu wengine ambao wamekuja na wamepata manufaa. Kwa hivyo, ni muhimu hasaa tuangalie upande wa uchumi na kuendeleza mbele kaunti hizi husika, ambazo Bandari ni jambo muhimu kwao, ni jambo linatakana kuangaliwa. Hata kama SGR iko na bidhaa nyingine itatolewa, lazima tuangalie njia vipi ajira itabaki pale pale nyumbani, vipi biashara itaendelea, hawa vijana ambao wanakuzwa kila siku, Mombasa, Kilifi, Kwale; watatafuta kazi wapi? Bi. Spika wa Muda, hili ni jambo sugu na nafikiri ni lazima tulitazame kwa umuhimu na umakini. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}