GET /api/v0.1/hansard/entries/886563/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 886563,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/886563/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, the Senate Majority Leader lazima aongoze kwa mfano. Yeye akiwa wa kwanza ku-consult kwa sauti inakuwa ni matatizo kwetu sisi wengine. Tulimskiza tukiwa kimya. Bw. Spika, marehemu Dkt. Ali Juma Hamisi alikuwa ni daktari katika zahanati ya Likoni mjini Mombasa akiwa ameajiriwa na Kaunti ya Mombasa, mpaka alipoenda Cuba mnamo tarehe 24 mwezi wa tisa mwaka uliopita. Madaktari wale waliuliza mambo matatu kabla ya kusafiri. Walitaka kujua ni c ourse gani walikuwa wanaenda kusomea. Pili walitaka kujua watakapoishi na tatu, marupurupu yao yatakuwa namna gani. Mambo hayo hayakujibiwa mpaka juzi tarehe nne wakati Wizara ilipeleka barua kusema kwamba watalipwa marupurupu ya Kshs33,000 kwa mwezi kuanzia mwezi wa tisa mwaka wa 2018. Bw. Spika, mpaka juzi, tarehe nne, walikuwa wamelipwa marupurupu ya miezi miwili pekee yake; mwezi wa tisa na mwezi wa kumi mwaka wa 2018. Mbali na kukosa marupurupu mahali wanapoishi haparidhishi. Hakuna internet wala mawasiliano mazuri baina ya familia zao na madaktari walioko kule Cuba. Kwa hivyo, hali zao za maisha zilikuwa zimerudi chini kuliko vile ambavyo walikuwa wanaishi hapa Kenya wakati wanafanya kazi serikalini na kaunti tofauti tofauti nchini Kenya. Kwa hivyo, swala hili ni zito sana na ni lazima litiliwe uzito, kwa sababu maisha yamepotea katika hali ambayo ni ya utatanishi. Marehemu Dkt. Ali alikuwa arudi nyumbani jana Jumanne, tarehe 19. Alikuwa ameshakata tiketi na kuzungumza na familia yake kwamba alikuwa anarudi siku hiyo. Kwa hivyo, lazima Serikali ichunguze swala hili na Bunge hili limuite Waziri wa Afya pamoja na maafisa wetu wanaosimamia mambo ya ubalozi, ili kuhakikisha kwamba hakuna jambo lolote mbaya lilitokea kabla ya marehemu kupoteza maisha yake."
}