GET /api/v0.1/hansard/entries/886571/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 886571,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/886571/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, chama cha madaktari walikuwa wamekataa mkataba huu na kusema kwamba hawaukubali kabisa, lakini Serikali ikaonelea ni lazima iendelee nao. Hatimaye ikafaulu na ikaona ya kwamba lazima wale madaktari waje. Walikuja na wakakaribishwa kitajiri, kama vile wenzangu wamesema. Mtu akikataa na umlazimishe, basi Waswahili husema: “Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.” Hii ndio faida tunayoipata hivi sasa, kuona ya kwamba sisi kama wakenya tulikuwa wapumbavu, tukaingia katika mkataba ambao haufai na hatimaye, tumempoteza daktari mmoja. Wizara ya Afya inayoongozwa na Cecily Kariuki ndio iliwafanya wale madaktari waende kule. Je, Waziri huyu amesema nini mpaka leo kuhusu kifo cha yule daktari? Mbona amekuwa bubu? Kama Waziri Cecily Kariuki ameshindwa na hii kazi ya Waziri wa Afya katika Kenya, atoke na kuwaachia madakatri wengine wafanye hio kazi. Bw. Spika, habari zinazotufikia hapa ambazo ni za ukweli kuhusu madaktari ambao wako kule Cuba ni kwamba wanaishi wanaume watatu ndani ya room moja. Mwanaume kama mimi na ndugu yangu, Sen. Sakaja, hatuwezi kulala katika chumba kimoja kwa sababu hairuhusiwi kiafrika."
}