GET /api/v0.1/hansard/entries/886573/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 886573,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/886573/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mimi na ndugu yangu, Sen. Wambua, hatuwezi kulala kwenye chumba kimoja; hairihusiwi kiafrika. Itakuwaje madaktari, ambao ni watu waliohitimu na wameenda kufanya masomo ya juu, wanaishi katika hali ambayo si ya binadamu? Si kiafrika kwa wanaume watatu kulala kwenye room moja. Kama watu wa Cuba hufanya hivyo, hapa kwetu Kenya haiwezekani mimi na ndugu yangu, Sen. (Eng.) Hargura, kulala kwenye room moja. Kwa hiyo, tunasema, heshima, lazima ilegeshwe na heshima. Ikiwa mkataba huu hauna heshima, sioni faida Serikali ya Kenya iendelee kuwa na mkataba huu baina ya sisi na wenyeji wa Cuba. Wale madaktari walio kule Cuba, kabla hatujapoteza mtu mwingine, waweze kurejeshwa nyumbani. Kuna ripoti ya kwamba, huyu ndugu yetu, Ali, alikuwa amesema amechoka na mateso yale na alitaka kurudi nyumbani lakini alitishiwa maisha yake. Daktari yeyote ambaye alikuwa anaweza kusema anataka kurudi nyumbani; walikuwa wanatishwa. Hata wakienda katika ubalozi wetu kule; walikuwa wanatishwa! Waliambiwa kuwa hawezi kuukata mkataba huu, hadi umalizike. Kwa hiyo, Bw. Spika, ikiwa inawezekana, kamati ambayo itachunguza jambo hili, ichukue msimamo wa kikamilifu kuona ya kwamba wamejadiliana na wamepata suluhu. Sisi tunasema ya kwamba; ni lazima Waziri wa Afya katika Serikali ya Kenya, aweze kuweka msimamo kama mkataba huu utaendelea, ama utakwatwa mara moja ili madaktari wetu warudi nyumbani, badala ya kuteseka kule Cuba. Hatutaki tena mambo ya Cuba. Asante sana, Bw. Spika."
}