GET /api/v0.1/hansard/entries/88721/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 88721,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/88721/?format=api",
    "text_counter": 493,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika ninakushuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kuunga mkono Hoja inayosema kwamba Bunge liende likizo hadi mwisho wa Septemba. Ningependa kuangazia mambo ambayo Bunge la Kumi limefanya. Wabunge katika Bunge hili wameshirikiana na kupitisha Miswada muhimu sana. Ingawa hivyo, tumefika wakati ambao lazima taifa liangazia mambo muhimu ya kuwaleta Wakenya pamoja. Kwa sasa tunasikitika kwa sababu serikali ya mseto inaonyesha dalili ya kutoelewana. Hii ndiyo inaleta kutoelewana kati ya wananchi. Ningependa kuomba serikali hii ya mseto ikiongozwa na viranja wawili kwamba ni muhimu serikali yao iongee kwa sauti moja. Katiba mpya imepitishwa. Mimi niliipinga lakini Wakenya wakaiunga mkono. Mimi ni miongoni mwa wale wanaoshukuru kwa sasa kuwa Kenya imepitisha Katiba mpya. Tunaiunga mkono kwa sababu tayari ni Katiba ya taifa la Kenya. Jambo muhimu ni utekelezaji wa Katiba hii. Tukio lililotokea wakati Katiba mpya iliidhinishwa ni la kuhuzunisha. Nimemsikiza Mhe. Karua akisema kwamba Wakenya wana haki kulingana na demokrasia ya kuonyesha hisia zao na hata kuzungumza. Ikiwa leo kiongozi kutoka Kenya ataenda kuhudhuria mkutano wa kitaifa kule Uganda, sisi Wakenya tutahisi vipi kama atakemewa katika huo mkutano ama aambiwe afunge virago vyake aelekee kwake? Sisi viongozi tuna mashabiki. Huu ni wakati wa kuwaambia kwamba kuna umuhimu wa taifa lakini vile vile kuna umuhimu wa kujumuisha mataifa yote ili Kenya iweze kuheshimiwa. Kenya imeonyesha tabia mbovu kupitia viongozi wao kwa tendo la kumkemea Rais wa taifa jingine. Kuna Wakenya wengi kule Sudan. Mimi nina ndugu"
}