GET /api/v0.1/hansard/entries/88722/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 88722,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/88722/?format=api",
"text_counter": 494,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kutuny",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "mmoja anayefanya kazi kule. Alinipigia simu na akanieleza kwamba tangu taifa letu litoe masharti kufuatia usafiri wa Rais wa Sudan humu nchini, vuta nikuvute ambayo iko humu nchini imewapa wasiwasi, hata wengi waliogopa kulala jana. Leo hawajui ni nini kitajiri. Hawajui kutatokea nini kesho. Tungependa Serikali iombe msamaha Rais wa Uganda. Pia, tunataka Serikali ya Kenya iombe msamaha Serikali ya Sudan ili sisi na Wakenya walio huko wapate kuheshimiwa. Kuna wanafunzi wengi Wakenya ambao wanasomea Uganda. Katika eneo bunge langu kuna wanafunzi 7,800 wanaosomea katika vyuo vikuu vya Uganda. Hao wanafunzi walianza kutishwa baada ya Rais Museveni kukemewa katika uwanja wa Uhuru Park. Serikali ichukue nafasi hii tunapoenda likizo itume kamati maalum kwenda kuomba msamaha katika nchi ya Uganda ili uhusiano wetu na wa mataifa uendelee kuimarika. Ningependa kuambia Serikali kwamba Kenya ni taifa huru. Kwa hivyo, kama kuna viongozi wachache ambao baada ya kuidhinisha Katiba wanataka kujipendekeza kwa mataifa yalioendelea, tunataka kuwaambia kuwa hiyo ni pilipili ambayo sisi hatuili na haituwashi. Kenya ina masharti yake na kiongozi wake ambaye ni Rais na lazima aheshimiwe. Tunataka kueleza mataifa yalioendelea: Tafadhali mtupatie nafasi sisi tumlee mtoto wetu anayeitwa Katiba mpaka akomae ili Wakenya waweze kuambatana na kuendelea. Ninataka kushukuru Serikali ya Marekani ambayo kwa sasa inataka kufanya mabadiliko ya balozi wake ambaye anawakilisha taifa hilo hapa Kenya. Nafikiri sasa imefika wakati ambapo sisi wengine tutasherehekea kwa sababu yule, kila wakati tukitengeneza mchuzi anakuja kuongeza ama kupunguza--- Afunganye virago na tunamtakia heri na fanaka popote atakapoenda. Yeye apeleke ujeuri wake na tuletewe mtu mwingine ambaye atawakilisha nchi ya Marekani hapa Kenya kwa heshima. Bw. Naibu Spika, naunga mkono."
}