GET /api/v0.1/hansard/entries/88729/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 88729,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/88729/?format=api",
    "text_counter": 501,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Asante Bwana Naibu Spika. Nasimama kuchangia Hoja hii ya likizo ya Bunge. Ningependa kuanza kwa kusema kwamba tuna taifa mpya baada ya kupitishwa kwa Katiba mpya. Taifa hili mpya haliwezi kuwa na maana kamwe kama bado tuna wananchi ambao wanateseka. Tukisema tuna Katiba mpya, tunamaanisha tuna nchi mpya na kuna uhuru wa wananchi wa Kenya. Vile mambo yalivyo sasa, wengine wanafurahia na wengine wanalia. Wale wanaolia ni wale tunaowaita wakimbizi wa ndani wa kisiasa ambao walifurushwa kutoka kwa mashamba na manyumba yao. Watu hawa hawakuwa na hatia lakini bado wanateseka. Hilo ni jambo ambalo linafaa kuzingatiwa na Waziri anayehusika ili tukirudi hapa, tuhakikishe kwamba kila Mkenya anafurahia uhuru wa nchi yake. Jambo la pili ni kwamba hatuwezi kuwa na Taifa mpya kama bado tunazungumzia ukabila. Tutakapoenda katika likizo, itakuwa ni jukuma la kila Mbunge kuhubiri amani na umoja wa Wakenya. Hatutaki kusikia ni wakati wa Wakalenjin. Hatutaki kusikia eti Wakikuyu wanangoja. Hatutaki kusikia ni njia ya Wakamba. Hatutaki kusikia sasa ni wakati wa Wajaluo ambao hawajakalia kiti. Tunataka kusikia kila kiongozi katika kila pembe ya nchi akisema kwamba tumevuka ule ukoloni wa ukabila na sasa tuko katika taifa mpya, Katiba mpya na tunataka kuwa Wakenya. Jambo lingine ambalo halifai kabisa ni hili: Haifai kumwarika kiongozi na akija hapa kwenye uwanja, anachekelewa. Anapigiwa kelele. Anaondoka hapa kurudi kwake ambapo kuna Wakenya. Nimepata simu kutoka ndugu zetu ambao wanaishi Uganda na wakaniuliza: “Mbona mlimualika Rais Museveni na kisha mkampigia kelele? Je, mnataka hapa tufanye nini?” Sisi hatuna haki au jukumu lolote la kuwaambia Wazimbabwe wasimuweke Mugabe. Kitu ambacho tunaweza kufanya ni kuwashauri na"
}