GET /api/v0.1/hansard/entries/88730/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 88730,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/88730/?format=api",
    "text_counter": 502,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "kuwaambia wazingatie demokrasia. Ni jukumu la Watanzania na Wasudan kuwalinda viongozi wao. Hata kama ni kichaa, ni jukumu lao. Sisi kama Wakenya hatuna uwezo wowote wa kuingilia maswala ya nchi nyingine. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa kiongozi ambaye tulimualika hapa na kumpa ulinzi kumpigia kelele. Wakenya wanafaa kujitunza na kuwa na heshima zao. Makasisi pia walipigiwa kelele. Ni demokrasia na ni lazima ionekana kwamba kila mtu anaheshimika kwa fikira na uamuzi wake. Bw. Naibu Spika, ni lazima tumheshimu Askofu Njue hata kama alipinga Katiba mpya. Sasa yeye ameikubali Katiba kama kiongozi wa dini. Ilikuwa ni jambo la aibu kuona watu wakimkemea Askofu Njue alipohudhuria sherehe ya kuidhinishwa kwa Katiba mpya. Ushindi huu si wa kikundi kimoja au chama cha kisiasa. Huu ni ushindi wa Wakenya wote. Demokrasia huhitaji maoni ya wachache kuheshimiwe. Bw. Naibu Spika, ilikuwa ni aibu kubwa kumuona Kadhi Mkuu akipigiwa kelele alipokuwa akiomba. Baadhi ya watu walitaka ayafupishe maombi yake. Jambo hili lilitendeka mbele ya Rais wa Zanzibari ambaye ni Muislamu na anaelewa lugha ya Kiswahili vizuri sana. Rais Al-Bashir haelewi lugha ya Kiswahili. Baadhi ya umati wa watu walitaka Kadhi Mkuu ayafupishe maombi yake. Ni dhahiri kuna watu katika nchi hii ambao hawamheshimu Mungu. Tuwasihi wafuasi wetu kumheshimu Mungu. Kwa hayo, ninaunga mkono."
}