GET /api/v0.1/hansard/entries/892252/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 892252,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/892252/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo inaomba Serikali itengeneze sheria ya kuwezesha viongozi wa Nyumba Kumi na viongozi wa vijiji kulipwa marupurupu. Kwa muda mrefu, hawa watu wamefanya hii kazi bila malipo yoyote. Wazee wa mtaa wanasaidia sana. Ukipatikana na shida huko kijijini ama ukipata wageni, mzee wa mtaa anajua. Pia, wanasaidia watu kupata vitambulisho. Wanajua nani hajapata kitambulisho. Pia, jambo lolote linapofanyika kijijini, kama matanga, wanawakusanya watu pamoja ili kupata namna ya kuwasaidia walioadhirika. Hii ni fursa nzuri kwetu tulio ndani ya Bunge hili linaloheshimika la kitaifa kuhakikisha kwamba Serikali imetengeneza sheria ya kulipa wazee wa mtaa, viongozi wa Nyumba Kumi. Pia, inafaa tutenge pesa katika Bajeti za kuhakikisha kwamba jambo hili limetendeka. Tukiongea na kusema wakasa, wazee wa mtaa na viongozi wa Nyumba Kumi walipwe bila kuhakikisha kwamba tumetenga pesa katika Bajeti ya nchi, itakuwa kazi bure. Kwa hayo, ninaunga Hoja hii mkono kwa sababu ni muhimu sana. Pia, ninatarajia kwa kipindi kifupi sana hizi pesa zitapatikana na wazee wa mtaa huko vijijini watapata marupurupu yao. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}