GET /api/v0.1/hansard/entries/892259/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 892259,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/892259/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Igembe South, Independent",
    "speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
    "speaker": {
        "id": 1574,
        "legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
        "slug": "cyprian-kubai-iringo"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii ambayo itawasaidia sana wazee wanaosaidia kule vijijini. Wazee hao huwa wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba tuna usalama wa kutosha na hakuna kitu wanachopata. Ndiposa asubuhi ya leo ninauliza Serikali iangalie na iweke mikakati mwafaka ya kuwasaidia wazee wa vijiji. Hii ni kwa sababu wazee hao wanajitolea kufanya kazi ambayo saa ingine inahatarisha maisha yao. Hili ni jambo ambalo Serikali yafaa kulishughulikia. Wakati kama huu Serikali inasema kwamba watoto wote wanafaa kwenda shule za sekondari. Wazee hawa huhakikisha kwamba watoto hao wamejiunga na shule. Wakati ambapo kuna migogoro katika vijiji vyetu na watu kupigana, ni wazee hawa ambao wako katika msitari wa mbele kwenda kushughulikia mambo haya au kuwafanya watu hao washirikiane kwa pamoja ili mizozo iweze kuondolewa. Serikali ina jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba wazee hao wanapata hela angalau za kuwafanya wasikie kwamba Serikali inawashughulikia wakati ambapo wanafanya kazi hii. Vilevile, ningeomba Serikali pia iwapatie wazee hawa ambao wanasaidia kule vijijini sare ili wakati wanafanya kazi hii, wajue kwamba Serikali inawashughulikia. Pia ikiwezekana wawe na afisi ambapo wanafanyia kazi kwa sababu wazee hao ndio walio karibu na wananchi wenye shida au mahali kwenye mambo yanayoleta kutoelewana katika vijiji. Wakati huu gharama ya maisha imeenda juu. Vilevile wakati wazee hawa wanapofanya kazi hii…"
}