GET /api/v0.1/hansard/entries/892277/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 892277,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/892277/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Turkana Central, ODM",
"speaker_title": "Hon. Lodepe Nakara",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": " Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kuungana na wenzangu ambao wameunga mkono Mjadala huu vilivyo. Sera ni kanuni ambazo zinatusaidia kufanya uamuzi ulio bora. Hatuwezi kuwasaidia wazee wa mtaa kama hakutakuwepo na sera ambazo zitawalinda na kuwafaidi. Ili kuwasaidia wazee, ni lazima tuwe na sera ambazo zitakuwa sheria na zitafuatwa kikamilifu ili baada ya Serikali yoyote kuingia ama kutoka, tutakuwa tumeweka sera ambazo zitawasaidia wazee. Tunahitaji sera ambazo zitakuwa sheria ili Serikali iwajibike kwa ajili ya wazee. Tusipokuwa na sera, itakuwa vigumu kufanya Serikali kuwajibika. Hiyo ndiyo sababu Bunge hili lazima litengenenze sera ili Serikali isipowalipa wazee, tunaweza kuipeleka Serikali kortini kwa sababu tutakuwa na sera ambazo tumeziweka. Sera hizi zitashughulikia mahitaji yote ya wazee. Hawa wazee wanafanya kazi kubwa sana katika vijiji vyetu. Hawa wazee ndio hakimu katika vijiji, wanatoa uamuzi ulio bora na wanaleta amani katika vijiji. Sera hizi ambazo tunaziweka katika Bunge hii lazima ziwasaidie wazee hao. Sio tu fedha peke yake. Tunataka Serikali iweke sera ambazo zitazawadi wazee hao. Kuna wengine ambao hawajawahi kufanya kazi maisha yao yote na hawana bima ya maisha na pesa za uzeeni. Kwa hivyo, tukiajiri hawa wazee, itabidi Serikali pia iwazawadi kwa kuwapatia mashamba ili wajijengee nyumba ama Serikali iwajengee ili waishi maisha ambayo ni mazuri."
}