GET /api/v0.1/hansard/entries/892354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 892354,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/892354/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Cherangany, JP",
"speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": " Nashukuru sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Awali kidogo nilikuwa na wasiwasi kwa sababu nimekitegea sana hiki kidude. Nashukuru kwa fursa umenipa. Wazee wa mtaa ni uti wa mgongo wa taifa. Kwa masuala ya kuunganisha jamii, wao ndio uso wa Serikali. Hawa ndio wanashughulikia masuala ya usalama wa kijamii. Matatizo yakiwepo kwa jamii, wao ndio huleta watu pamoja. Serikali ilipoanzisha Nyumba Kumi, ilikuwa inategemea wazee wa mtaa waishughulikie. Lakini ukiangalia hali yao, wamezorota. Ukiangalia jinsi machifu na wakubwa wengine wa Serikali wanashughulikiwa, utashangaa jinsi wazee wa mtaa wameachwa bila kushughulikiwa. Wao pia wana watoto wanaowasomesha. Vilevile wana makao, lakini ukiangalia makao yao, hayastahili watu ambao wanafanya kazi kwa Serikali. Vilevile wana famila za kutunza na kupatia chakula. Afya ya wengi imezorota. Hatua za Serikali za kuimarisha hali yao duni ni kama kusema; “kufa kwa inzi kidondani sio hatia.” Hata hii haingekuwa Hoja. Ungekuwa Mswada ili tuitunge sheria kama Bunge kushurutisha Serikali kuwalipa wazee wa vijiji kama wafanyikazi wengine was Serikali. Kwa hivyo, naunga mkono wenzangu kwamba Hoja hii tuipigie kura ya upato tukitarajia kwamba Serikali itaitilia maanani. Tatizo ni kwamba Hoja inazungumziwa hapa lakini haishughulikiwi. Kwa hivyo natarajia kitengo husika ndani ya Bunge kitaweza kusukuma Serikali iweze kutilia maanani matakwa ya hawa wazee wa mtaa. Nashukuru."
}