GET /api/v0.1/hansard/entries/892364/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 892364,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/892364/?format=api",
    "text_counter": 271,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Baringo South, JP",
    "speaker_title": "Hon. Charles Kamuren",
    "speaker": {
        "id": 1202,
        "legal_name": "Charles Kamuren",
        "slug": "charles-kamuren"
    },
    "content": " Asante Mheshimiwa, Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii ya kuwalipa mishahara viongozi wa mitaa na vijiji. Ni vyema Serikali iwashughulikie kwa sababu wanafanya kazi nzuri. Wakati mwingi wao ndio wanaoishi na wananchi. Wanasaidia Serikali sana. Kwa hivyo, ni vyema wapewe mishahara na sare rasmi ili watambulike. Inafaa pia wapewe vitambulisho na simu za rununu ili wakiwa na shida wapige simu na kusaidiana na viongozi wengine. Pia, inafaa wapewe fimbo za mamlaka. Kwenye utawala nchini Kenya kuna fimbo ya mamlaka. Hiyo itawafanya waonekane viongozi."
}