GET /api/v0.1/hansard/entries/892375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 892375,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/892375/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Dennitah Ghati",
"speaker": {
"id": 856,
"legal_name": "Dennitah Ghati",
"slug": "dennitah-ghati"
},
"content": " Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, nashukuru sana kwa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii iliyoletwa hapa na Mhe. George Murugara. Hii ni Hoja ambayo imenifurahisha sana. Kule vijijini tunakotoka, watu wanaohakikisha kwamba amani inadumishwa, na kuhakikisha kwamba jamaa wetu wanaishi katika hali ya heshima, ni wazee wa Nyumba Kumi au liguruu . Tunaunga mkono Hoja hii ili Serikali kuu iwajumuishe kwenya orodha ya wafanyikazi wa umma wanaolipwa mishahara. Niruhusu niseme kwamba hawa watu wetu ni lazima walipwe mishahara kila mwisho wa mwezi. Hii ni kwa sababu kazi ambazo wanafanya pale chini ni kazi ambazo ni za kudhalilishwa tu. Hawa wazee walipwe kila mwezi na tunapoongea juu ya hawa village elders, lazima tujue ya kwamba hawa viongozi wetu ambao ni wazee wa Nyumba Kumi wao pia ni wamama wa Nyumba Kumi. Unapoona vile tunaongea tunasema tu juu ya wazee wa Nyuma Kumi na hii ni jinsia moja. Tukiendelea kujadiliana, tuhakikishe kwamba hata wamama pale nyumbani wanahusishwa kama viongozi wa Nyumba Kumi ili tuwe na gender balance kwa sababu hii ni kazi muhimu."
}