GET /api/v0.1/hansard/entries/892394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 892394,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/892394/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala huu kuhusu wazee wa mtaa. Kwanza, ninachukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Murugara kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili. Miaka miwili iliyopita, tulikuwa na Hoja kama hii katika Bunge hili na hakuna mabadiliko yoyote yalitendeka. Ninafikiria leo tunapojadili Hoja hii, tutahakikisha kwamba imetekelezwa vilivyo kwa sababu vile wenzangu wamechangia katika Bunge hili, ni kweli wanafanya kazi nyingi sana. Katika utoaji wa vitambulisho, wazee hawa wanachukua nafasi ya maana sana kuwatambua wenyeji katika vijini wanavyotoka. Pia wana majukumu makali sana hasa ikija katika mambo ya ugomvi wa nyumbani kina mama wanapogombana au watoto waliowashinda wazazi wao. Hawa huenda kwa wazee wa mtaa kuhakikisha kwamba wanaleta maridhiano miongoni mwao. Kama Mhe. Dennitah Ghati alivyosema, miongoni mwao mna kina mama wanaodhulumiwa kwa sababu wanapopewa kesi za kufanya katika vijiji hivyo, wengine wananajisiwa. Pia wanatakikana wapewe usalama kwa sababu wanatembea bila vifaa vyovyote vya kuwakinga kama machifu wanavyopewa. Vile wenzangu wamesema ni kweli. Tunapotengeneza Bajeti, angalau tutenge pesa za kuhakikisha kwamba hawa pia wanapata pesa za kukidhi jamii zao. Katika baadhi ya kaunti, kuna magavana waliojitolea kuhakikisha kwamba wazee wa mtaa wanaishi vizuri lakini wengine hawajui maana ya wazee hawa wa mtaa kwa sababu walipata kura kwa njia ambayo haieleweki. Ninaunga mkono Hoja hii angalau wazee wa mtaa wapewe senti kidogo. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}