GET /api/v0.1/hansard/entries/893623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 893623,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/893623/?format=api",
    "text_counter": 15,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika. Ninaungana nawe kuwakaribisha wanafunzi wa kutoka Lamu na vijana kutoka Kakamega. Awali nilipata fursa ya kuongea nao na kuwapa motisha katika shughuli zao za kuendeleza mambo ya masomo, hasa wale waliotoka upande wa Kakamega kwa kuwa wanasomea kuwa mapadri. Niliwaambia kwamba mimi kama Mkatoliki ninajua kwamba kuna ule ugumu wa kusomea kuwa padri, lakini nikawaambia ya kwamba ni vizuri wajitie moyo na ninahakika kwamba, wakijifunga kibwebwe, wataweza kupasi masomo yao. Wanafunzi kutoka Lamu nao niliwaambia kwamba ninajua wametoka mbali ndipo waweze kuja hapa kuona vile ambavyo tunajadili mambo hapa Seneti. Niliwaambia kuwa kile ambacho ni cha manufaa kwao ni masomo. Masomo ndio uti wa mgongo wa maendeleo katika nchi yetu ya Kenya. Wao kama vijana ndio---."
}