GET /api/v0.1/hansard/entries/895130/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895130,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895130/?format=api",
    "text_counter": 337,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Ningependa kumpongeza Rais pia kwa kuunga mkono na kutoa hakikisho kwamba ile hatua ya ujengaji madaraja, yaani, “ Building Bridges Initiative ” itaendelea kuwa, kwa sababu imeweza kuleta amani kwa muda mchache ambao tumekuwa nao - karibu mwaka mmoja. Alisema kwamba ataendelea kuiunga mkono kwa sababu ni njia ambayo inawaleta Wakenya pamoja. Joto la kisiasa limeweza kupungua licha ya wale ambao wanatangatanga wakitafuta kuungwa mkono kwa ugombezi wa Rais wa mwaka wa 2022, ambao kwa sasa sio muhimu kwa nchi. Cha muhimu sasa hivi ni kuweza kujenga nchi ili wananchi wapate fursa ya kupata kazi, biashara ziweze kuinuka na pia tuwe na usalama katika Jamhuri yetu ya Kenya."
}