GET /api/v0.1/hansard/entries/895131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895131,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895131/?format=api",
    "text_counter": 338,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, tangu mkataba au mwafaka upatikane baina ya Rais Kenyatta na „Rais wa wananchi,‟ Mhe. Raila Amolo Odinga, joto la siasa limepungua. Wananchi wanaweza kufanya kazi, biashara zimeanza kufunguka na vile vile, hali ya uchumi wa nchi imeweza kupanuka na kufunguka. Biashara hususan katika Mji wa Mombasa zimeanza kuinuka, na hilo ni jambo nzuri kwa sababu ugatuzi unategemea pakubwa biashara katika maeneo yale, ili waweze kupata ushuru na kuinua hali ya maisha ya watu."
}