GET /api/v0.1/hansard/entries/895136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895136,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895136/?format=api",
    "text_counter": 343,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Tunatarajia kwamba pendekezo litafanywa kesi za ufisadi ziweze kukamilishwa kwa muda wa miezi sita kama vile kesi zinazohusu uchaguzi. Kesi hizi zikiendelea kukaa katika mahakama, washtakiwa wanapata fursa zaidi ya kujinasua na mwisho mashahidi wanapotea. Kwa hivyo, wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanaepuka kifungo ama adhabu kwa sababu hakuna ushahidi. Kwa hivyo, mahakama inapaswa iongeze dhamana ili tuhakikishe kwamba vita dhidi ya ufisadi inapamba moto. Nilisikitishwa kwamba Idara ya Kiongozi wa Mashtaka ya Serikali pamoja na Idara ya Upelelezi yani (DCI) haikupewa mwongozo wowote na Serikali kuhusu ni jambo gani wataweza kufanyiwa ili kuhakikisha kwamba uchunguzi unafanyika kwa haraka na stakabadhi za mahakama ambazo zinatakikana kupelekwa kortini zinapelekwa kwa wakati unaofaa. Bw. Spika wa Muda, ijapokuwa Tume ya Kupigana na Ufisadi inafanya kazi kubwa, kesi ambazo zinahusiana na mambo ya ufisadi zimekuwa nyingi. Kwa mfano, katika kila gatuzi katika nchi ya Kenya, kufuatia ripoti za Auditor-General utapata kwamba katika kila kaunti kuna swala la ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za kauti au utumizi mbaya wa mamlaka. Kwa hivyo, tukihesabu kwamba kila kaunti ina kesi, ina maana kwamba, hivi sasa, maafisa wa ufisadi wanaweze kuwa katika kila kaunti. Kwa sasa, ofisi zao ziko katika ofisi za zamani za mkuu wa mkoa, kama vile, Mombasa, Embu, Garissa na kwengineko. Kwa hivyo, lazima tuongeze maafisa wanaofanya uchunguzi kwa Idara Ya Upelelezi na pia Tume ya Kupigana na Ufisadi. Jambo lingine ambalo lilinitamausha ni kuwa ripoti ya hali ya usalama haikutiliwa maanani, kama vile watu kuolewa na kuuliwa kiholela na watu wa Serikali ama makundi ya kigaidi kama vile, Al shaabab na makundi mengine ambayo yanafanya mauaji ya kinyama katika sehemu tofauti tofauti. Kwa mfano, katika eneo la Mombasa, kuna makundi katika maeneo ya Likoni na Kisauni. Wengine wanajiita watoto wa bibi, jukuu wa babu na kadhalika. Makundi haya ni ya kigaidi. Wanafanya unyama. Wanakata watu kwa mapanga na kuwaua bila hao kuwa na hatia yeyote. Serikali inafaa kuchukulia hatua vikundi kama hivi kwa sababu maafisa wa polisi pia hawakusaswa katika mauaji kama haya. Bw. Spika wa Muda, jana tulikuwa na kikao maalum cha Kamati ya Haki na Sheria mjini Mombasa ambapo tulipata ripoti kwamba zaidi ya watu 45 wameuliwa. Baadhi yao ni wazee wa mitaa ambao wamepewa majukumu ya kuangalia mambo ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}