GET /api/v0.1/hansard/entries/895137/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895137,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895137/?format=api",
    "text_counter": 344,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "mtaa na usalama. Kwa hivyo, ikiwa wazee kama hawa watauliwa, itakuwa ni vigumu kwa vyombo vya Serikali kupata habari kuhusu mambo ya mitaa inavyokwenda. Bw. Spika wa Muda, tumeelezewa kwamba zaidi ya watu 15 katika eneo la Kwale wamepotea. Mombasa vile vile, zaidi ya watu 90 wamepotea na wengine wengi wameuawa katika hali za kutatanisha. Tumekubaliana kwamba nchi lazima iongozwe kwa sheria. Iwapo watu watauawa kiholela, inamaanisha kwamba imani kwa Serikali kulinda mali na maisha ya watu itapungua. Kwa hivyo, kuna hatari ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao na kusababisha maafa bila ya kujua kwamba Serikali ipo. Bw. Spika wa Muda, swala la watoto kupotea hususan katika maeneo ya Pwani kuanzia sehemu za Lunga Lunga, Kwale mpaka Lamu ni swala ambalo ni donda sugu katika nchi yetu. Inatakikana Serikali itoe mwongozo. Kama ni kweli kwamba watu wanawachukua, basi wanafaa kuwarejesha makwao na kuomba msamaha kwamba walishika watu na kuwaweka ndani bila kufuata sheria. Kulingana na sheria, mtu yeyote anaye tuhumiwa kwa makosa yoyote anatakikana kupelekwa mahakamani chini ya saa 24. Hosni Mubarak alishikwa mwezi wa tano mwaka jana na mpaka leo hajapatikana. Mwingine anayeitwa Helef Halifa alishikwa Novemba, 2017 na mpaka leo hajapatikana. Pia kuna mwingine anayeitwa Farah Abdi Farah aliyeshikwa 2015 na mpaka leo hajapatikana wala hajulikani alipo. Ni kama Serikali imewazuia watu hawa. Wanafaa kujitokeza wazi na kutuambia ukweli. Hata hivyo, endapo wafungwa wataomba msamaha, wanafaa kuachiliwa kwa sababu sheria inahitaji mtu apelekwe mahakamani. Katika vitengo vitatu vya Serikali, mahakama ndiyo ina uwezo wa kuamua mizozo baina ya Serikali na raia, na baina ya taasisi tofauti tofauti za Serikali. Kwa hivyo, watu hao wanafaa kupelekwa mahakamani ili Serikali iwajibike. Bw. Spika wa Muda, kuna baadhi ya maafa ambayo yana tokea. Kwa mfano, ulanguzi wa dawa za kulevya ni jambo ambalo limeathiri sana watu wa Mombasa na Pwani kwa jumla. Ijapokuwa Serikali imejipiga kifua kwamba inafanya kila iwezalo kuhakikisha kwamba ulanguzi wa dawa za kulevya unaisha, kila siku watu hususan vijana wa umri wa chini ya miaka 18 wanaendelea kujiingiza katika dawa za kulevya. Hiyo inamaanisha kwamba Serikali haijaweza kujenga vituo vya kusaidia kuokoa vijana wanaojiingiza katika lindi la dawa za kulevya. Nafurahi kwamba juzi, shirika la Msalaba Mwekundu lilianzisha kituo cha kurekebisha tabia, yani rehabilitation centre, kule Lamu. Kituo hicho kitasaidia wagonjwa ambao wamejiingiza katika utumuzi wa dawa za kulevya. Serikali ina jukumu la kuhakikisha kwamba watu wake wanaishi kwa usalama. Ukosefu wa usalama umesababishwa na dawa za kulevya. Kwa hivyo, lazima tupambane na dawa za kulevya ili kuhakikisha kwamba watu wetu, hususan vijana wanaotumia dawa za kulevya, wanaishi maisha mazuri. Rais pia alisema kwamba reli ya Standard Gauge (SGR) imebadilisha usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Mombasa hadi Nairobi, na kwamba sasa mizigo inapelekwa haraka zaidi kuliko hapo awali. Tunaunga mkono SGR kwa sababu ni njia moja ya kusaidia nchi kukua. Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kwamba SGR imewapotezea watu wengi kazi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}