GET /api/v0.1/hansard/entries/895138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895138,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895138/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kwa mfano, zaidi ya madereva 6,000 pamoja na wasaidizi wao ikiwemo wanaofanya kazi katika vituo vya mafuta wamepoteza kazi. Vile vile, biashara nyingi zimefungwa kwenye barabara ya kutoka Mombasa kuja Nairobi, kuanzia Mariakani hadi Mlolongo. Watu wa sehemu hizo walikuwa wanapata pesa wakati mizigo mingi ilikuwa inasafirishwa kutumia barabara. Simaanishi kwamba SGR isitumike. Ninacho maanisha ni kwamba wenye lori watengewe sehemu za kubebea mizigo. Hapo awali, kulikuwa na kile ninachoweza kusema “uchumi uliofungwa” na hatimaye tukawa na soko huru ili kuwezesha kila mtu aweze kufanya biashara na marketforces ziliamua bei ya kuuza mali. Iwapo tutaruhusu mizigo yote ibebwe kutumia SGR, ina maana kwamba tutakuwa tunaendeleza ukiritimba ili kuzuia watu wengine kufanya biashara. Katika maeneo ya Mombasa, mashirika mengi ya kupakia na kupakua mizigo yamefunga kwa sababu mizigo mingi na makasha yote katika Bandari ya Mombasa yana safirishwa kutumia SGR."
}