GET /api/v0.1/hansard/entries/895139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 895139,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895139/?format=api",
"text_counter": 346,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, hatukatai kwamba kuna maendeleo lakini tunasema kwamba ni lazima biashara ifanywe kulingana na njia za haki. Hatuwezi kusema kwamba mizigo yote isafirishwe kwa reli kwa sababu reli kwa sasa haina uwezo huo. Iwapo mashirika ya biashara au wenye makampuni ya kusafirisha mizigo yatafunga biashara zile, watu wengi watapoteza kazi na vile vile, uchumi wetu utaathirika. Hii ni kwa sababu magari yote yanayosafiri yana nunua mafuta. Katika kila lita moja ya mafuta ambayo yanauzwa ambayo ni zaidi ya shilling mia moja, shilling 30 zinaingia kwa Serikali kama ushuru. Kwa hivyo, Serikali itapoteza ushuru, watu watapoteza kazi na bishara zitakufa. Kwa vile Serikali haina mpango mbadala wa kusaidia, ina maana kwamba watu wengi watapoteza biashara na uchumi utaathirika."
}