GET /api/v0.1/hansard/entries/895143/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895143,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895143/?format=api",
    "text_counter": 350,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Tumeona miradi mingi iliyoanzishwa na Serikali. Kwa mfano, katika Kaunti ya Tana River, wameanzisha mradi wa Galana-Kulalu. Mradi huo ulitakiwa upewe gatuzi la Tana River na Kilifi ili ufanywe kama mradi wa pamoja. Kama vile tunavyosema Kaunti ya Mombasa tupewe mradi wa Dongo Kundu Special Economic Zone ili uweze kusaidia kama biashara mbadala wa ile Bandari ya Mombasa ambayo kwa sasa inaondolewa pole pole. Ikiwa tutaruhusiwa kufanya Dongo Kundu Special Economic Zone, itasaidia pakubwa kuinua hali ya watu na uchumi wa Kaunti ya Mombasa. Hii ni kwa sababu watu watapata kazi, mizigo itaingia na watu watauza kama vile Dubai. Hiyo ina maana kwamba biashara itaweza kufunguka tena kwa mji wa Mombasa. Hali hii ya kaunti kuongojea ruzuku kutoka kwa Serikali kuu kila mwaka ina maana kwamba hazipewi fursa ya kukua. Inafaa kila kaunti ipewe nafasi ya kuinua uchumi katika sehemu zake. Sisi katika Kaunti ya Mombasa, njia kubwa ya kuinua uchumi ni kupewa mradi wa Dongo Kundu Special Economic Zone. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}