GET /api/v0.1/hansard/entries/895148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895148,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895148/?format=api",
    "text_counter": 355,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Biashara ya uvuvi inafanywa na mashirika makubwa ambayo yanatoka sehemu za nje. Hapa kwetu, wavuvi wengi wanatumia vifaa duni kama vile vihuri, uvuvi wa mishipi na uvuvi wa kienyeji ambao kwa hakika mapato yake ni machache sana. Kama itawezekana, inafaa Serikali itilie maanani suala la uvuvi. Itasaidia pakubwa kuinua uchumi wa watu wa Mombasa na Pwani kwa jumla."
}