GET /api/v0.1/hansard/entries/895643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 895643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895643/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia ombi lililoletwa na Sen. Dullo kuhusiana na unyakuzi wa ardhi na Jeshi la Kenya. Kusema kweli, sio Isiolo peke yake iliyo na shida hii; ni kama huu umekuwa mtindo ambapo mashirika ya Kiserikali yanachukua mashamba katika sehemu tofauti tofauti bila ruhusa. Kwa mfano, kule Taita-Taveta ninakotoka, maafisa wa Kenya Wildlife Service (KWS) wamechukua shamba la ekari 380 upande wa Mbololo na kulitafutia hatimiliki. Tumetafuta njia ya kurejesha ardhi hiyo kwa kaunti, lakini imekuwa shida. Hii ni kwa sababu ukiwa na hatimiliki, ili kuirudisha ardhi hiyo, lazima upitie mahakamani."
}