GET /api/v0.1/hansard/entries/895777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 895777,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895777/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Kwanza, naunga mkono Hotuba ya Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta aliyoitoa kwa Vyumba viwili vilivyokutana ndani ya Bunge la Kitaifa. Ninamshukuru Rais kwa kutoa Hotuba iliyogusa mambo mengi ambayo yana husika na wananchi ama ujenzi wa taifa. Kuna mengi ambayo Rais hakuguzia na ingekuwa vyema kama angeyaguzia. Jambo la kwanza na muhimu ni jukumu la Serikali kuona ya kwamba kazi kwa vijana imetekelezeka. Hii ni kwa sababu katika manyumba zetu vijana wengi wanaomaliza shule hawana kazi. Hakuna njia za aina yeyote ambazo Serikali imeanzisha ya kuona kwamba vijana hawa wamepata kazi. Bw. Spika wa Muda, hakuna hatari kubwa katika taifa lolote katika ulimwengu ikiwa watu wamehitimu wakapata shahada za degree lakini hawana kazi. Vijana kama hawa wana akili kwa sababu wamesoma na wanaweza kutumia akili zile kwa njia nyingi. Ndiyo maana watoto wetu wanaingia katika makundi ya Al Shabaab . Hii ni hatari kwa sababu vijana hawa wamesoma na wanaweza kukagua na kujua ni jinsi gani wanaweza kutenda kitendo ambacho Serikali inaweza kupata habari. Ilikuwa ni muhimu jambo kama hili liwe katika Hotuba ya Rais, lakini, Rais hakulitia mkazo. Hili jambo ni donda sugu ndani ya Serikali ya Kenya na nchi yetu. Bw. Spika wa Muda, jambo la pili ni kwamba Rais aliguzia mengi kuhusiana na makampuni lakini hakuweza kugusia mashirika ambayo watu walitumia njia za ufisadi na kufanya yapoteza mwelekeo na hatimaye yakafungwa. Ninazingatia ya kwamba kuna mashirika katika maeneo ya Pwani. Kwa mfano, Mmea wa korosho umekuza uchumi wa watu wa Kilifi na wengine wetu tumesomeshwa kwa huu mmea. Zamani, wazee walikuwa wanauza korosho kwa cooperative society na kupata karo ya shule. Bw. Spika wa Muda, ningependa kusisitiza ya kwamba kuna Bixa Factory ambayo ilikuwa inaleta pesa nyingi katika eneo la Kaunti ya Kwale lakini, hivi sasa, shirika hilo limepiga magoti na kufilisika. Vile vile, shirika la Ramisi Sugar limepiga magoti na kufa. Halifanyi kazi yeyote na watu wameachishwa kazi. Kwa hivyo, Rais angeweka mkazo zaidi kwa hotuba yake atakavyo fufua vitengo kama hivi. Zaidi, angeweka mkazo ya kwamba, katika ulimwengu hivi sasa, mmea wa korosho una manufaa sana. Bw. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha kwamba Hotuba ya Rais haikuweza kuweka kinagaubaga ni njia gani ataweza kufufua mashirika ambayo yalifilisika na kufilisishwa na watu ambao hivi sasa wako ndani ya Serikal na wengine wamestaafu. Vile vile, hotuba ya Rais iliguzia mambo mengi lakini kuna changamoto kubwa sana. Hivi sasa, kaunti zina lazimishwa kulipa pesa nyingi kwa sababu ya mashini ambazo zililetwa na Serikali Kuu kusaidia upande wa kupiga picha, kama vile, MagneticResonance Imaging (MRI), Xray na nyinginezo. Hatimaye, waliingia katika mkataba ili serikali za ugatuzi ziweze kuzingatia na kuweka vidole. Hizi pesa ni nyingi sana lakini mashini nyingi ziko hospitalini lakini hazifanyi kazi. Zimekaa kiholela. Kama zinafanya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}